Jumatatu 13 Julai 2026 - 14:00
Imam Shahidi Amedumisha Ujumbe wa Muqawama na Kuwatetea Wanaodhulumiwa Kwa Kuitoa Nafsi Yake Sadaka

Hawza/ Wanazuoni wa Bangladesh wamesema kuwa; Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Husseini Khamenei (ra), kwa kuitoa nafsi yake na familia yake sadaka katika njia ya Mwenyezi Mungu, ameonesha kwamba Uislamu kamwe hautasalimu amri mbele ya madhalimu, bali daima utasimama upande wa wanaodhulumiwa duniani.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla kubwa ya kumbukumbu na kuenzi maisha ya Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Husseini Khamenei (ra), pamoja na familia yake mashahidi, imefanyika katika mji wa Khulna nchini Bangladesh, ikihudhuriwa na wasomi, wanataaluma, viongozi wa kitamaduni na kijamii.

Hafla hiyo ilianza kwa kusomwa aya za Qur’ani Tukufu, kufuatiwa na Dua ya Faraj ya Imam wa Zama (aj), pamoja na dua ya kuombea heshima, utukufu na kuinuliwa kwa Umma wa Kiislamu.

Imam Shahidi Hakuwahi Kusalimu Amri Mbele ya Ujeuri na Uistikbari

Katika hafla hiyo, Dkt. Shah Jalal, mhadhiri wa Idara ya Lugha ya Kiajemi katika Chuo Kikuu cha Khulna, akizungumzia shakhsia na njia ya Imam Shahidi alisema: "Kosa la Imam Shahidi lilikuwa nini? Je, mbali na kuwatetea wanaodhulumiwa na kusimama dhidi ya dhulma, alikuwa na kosa jingine? Aliombwa ajiondoe katika uwanja wa mapambano, lakini alichagua kuutoa uhai wake katika njia ya malengo ya Mwenyezi Mungu na kufikia daraja ya shahada."

Akilinganisha njia ya Imam Shahidi na harakati ya Ashura, aliongeza: "Kama ambavyo Imam Hussein (as) aliutoa uhai wake kwa ajili ya kuhuisha wajibu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, vivyo hivyo Imam Shahidi aliendeleza njia hiyo kwa subira na uimara, na hakuwahi kamwe kusalimu amri mbele ya ujeuri na uistikbari."

Mhadhiri huyo pia alilaani mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran na kusema: "Kushambulia hospitali, vituo vya elimu na kuwaua wananchi wasio na hatia ni mfano wa wazi wa jinai dhidi ya ubinadamu."

Katika sehemu nyingine ya hafla hiyo, Jalaluddin, mwanaharakati wa kijamii, alisimulia jinsi alivyoanza kufahamiana na shughuli za kidini za Waislamu wa madhehebu ya Shia. Alisema: "Tangu mwaka 1980, baada ya kushuhudia moja ya majlisi za maombolezo, nilianza kushirikiana na Husseiniyya ya Khulna, na uhusiano huo unaendelea hadi leo."

Aidha, akizungumzia jinai za utawala wa Kizayuni nchini Palestina, alilaani mauaji ya halaiki ya watoto wa Kipalestina.

Vilevile, Dkt. Zakir Hussein, Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Khulna, alimuelezea Imam Shahidi kuwa alikuwa kiongozi wa kimapinduzi na mtetezi wa wanaodhulumiwa alisema: "Kwa kufuata njia ya Imam Hussein (as), aliudhihirishia ulimwengu kwamba Uislamu daima unasimama pamoja na wanaodhulumiwa na dhidi ya madhalimu."

Aliongeza kuwa; jumuiya ya wanasheria na mawakili wa Khulna imelaani mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, na kwamba ingawa baadhi ya serikali za Kiislamu zimechukua misimamo dhidi ya Iran, mataifa na Umma wa Kiislamu bado wanaendelea kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu na Muqawama.

Hadhi ya Kielimu na Kiroho ya Imam Shahidi

Katika mwendelezo wa hafla hiyo, Maulawi Abdul Rashid, aliyewahi kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Serikali cha Dhaka, alieleza mapenzi yake kwa Imam Shahidi kwa kusema: "Iwapo Mwenyezi Mungu ataniuliza: Umeifanyia nini dini ya Uislamu? Nitajibu kwamba nilimpenda kwa dhati Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Husseini Khamenei (ra), na nilihudhuria hafla za kumuenzi na kumuomboleza."

Akirejelea kazi zake za kielimu, alisema: "Baada ya kusoma tafsiri ya Suratul Taghabun aliyoiacha, nilistaajabu sana. Katika maisha yangu, sijawahi kuona mfasiri mwenye kina hicho cha kielimu na mtazamo makini wa Qur’ani isipokuwa wachache sana."

Baadaye, Maulawi Abdul Rahman, mmoja wa wanaharakati wa masuala ya utamaduni nchini Bangladesh, huku akizungumzia nafasi ya Imam Shahidi katika kuleta ukaribu kati ya madhehebu ya Kiislamu alisema: "Ayatullah al-Udhma Khamenei (ra) alitekeleza jukumu muhimu katika kuimarisha umoja kati ya Shia na Sunni, na daima aliuhimiza Umma wa Kiislamu kuwa na mshikamano na umoja."

Imam Shahidi; Mfano wa Kusimama Dhidi ya Dhulma

Abdul Quddus, mjumbe wa Baraza la Jamaat-e-Islami katika mji wa Khulna, alisema: "Ayatullah al-Udhma Khamenei (ra) alikuwa shahidi mkubwa zaidi, kiongozi mashuhuri zaidi na mmoja wa viongozi bora wa kisiasa wa zama hizi. Ingawa amepata shahada, malengo, maadili na misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hayajabadilika hata kidogo."

Aliongeza: "Imam Shahidi, kwa kuitoa nafsi yake na familia yake sadaka, amethibitisha kwamba Uislamu kamwe hautasalimu amri mbele ya madhalimu, bali daima utasimama upande wa wanaodhulumiwa."

Maisha ya Kawaida na Jihadi ya Imam Shahidi

Qassim Sheiban, mmoja wa maafisa wa Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu mjini Tehran, alisema: "Sababu ya madola ya kibeberu kumchukia Imam Shahidi ilikuwa ni msimamo wake thabiti dhidi ya ubeberu na ukoloni. Hata kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika kipindi cha utawala wa Pahlavi, alikabiliwa mara nyingi na mateso na shinikizo."

Aliongeza kuwa; wakati wa vita vya kulazimishwa vya Iraq dhidi ya Iran, Imam Shahidi alikuwa daima mstari wa mbele katika kuilinda nchi. "Maisha yake yalikuwa ya kawaida sana na mbali kabisa na anasa. Nyumbani kwake hakukuwa na vifaa vya gharama kubwa, sifa hizi zote zinaonesha kwamba siku zote alikuwa pamoja na wanyonge na mtetezi wa haki zao."

Sheiban pia aliwashukuru wananchi wa Bangladesh kwa ushiriki wao mkubwa katika hafla hiyo na kusema: "Nitaufikisha upendo na mapenzi ya wananchi wa Bangladesh kwa Imam Shahidi katika Ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu."

Sifa za Kielimu na Kimaadili za Imam Shahidi

Katika sehemu nyingine ya hafla hiyo, Mehdi Molaei Arani, Mshauri wa Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Bangladesh, alisema: "Imam Shahidi alikuwa tofauti na viongozi wengi wa kisiasa duniani, wakati alipopata shahada, alikuwa katika chumba chake cha masomo akifanya utafiti na kujisomea."

Aliongeza kuwa; masomo ya Imam Shahidi hayakuwa yamejikita katika elimu za dini pekee, bali pia alisoma kwa muda wote falsafa, elimu za jamii na taaluma nyingine mbalimbali. Aidha alisema kuwa; familia yake iliyopata shahada wote walikuwa watu wa kada ya elimu na walimu.

Akizungumzia roho yake ya kupambana na dhulma, alisema: "Daima alisisitiza kwamba Muumini wa kweli kamwe hasalimu amri mbele ya batili na dhulma."

Kuhifadhi Utamaduni Hai wa Shahada

Sayyid Mustafa Mousavi, mhadhiri na mtafiti wa Hawza ya Qum, alisema: "Imam Shahidi alikuwa akisisitiza daima kwamba; kuenzi kumbukumbu za mashahidi ni jukumu la kila mmoja, kwa sababu kuna makundi yanayojaribu kuufuta utamaduni wa jihadi, kujitolea na shahada kutoka katika nyoyo na fikra za watu."

Aliongeza: "Sote tuna wajibu wa kusimama dhidi ya njama hizo, kwa sababu mashahidi ni alama ya ikhlasi, kujitolea na kujitoa mhanga katika njia ya Mwenyezi Mungu."

Mwishoni mwa hafla hiyo, washiriki walisoma dua ya hitimisho na kumuomba Mwenyezi Mungu aujalie Uislamu heshima na utukufu, aujaalie Umma wa Kiislamu umoja na mshikamano, na awainue mashahidi katika daraja za juu kabisa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha